ELIZABETH Michael ‘Lulu’ mwigizaji wa kike mwenye nyota kali anasema
kuwa hawezi kwa sasa kuonekana kwa kila filamu bila sababu kwani
amejipanga kutafuta tuzo kubwa za kimataifa hivyo lazima ashiriki sinema
bora ili kufikia malengo yake.
“Kuwa bora si kucheza sinema nyingi bali kuwa na sinema za maana,
nimejipanga na nakuja na filamu yangu ya Ni Noma ni filamu kubwa sana
kutengezwa Afrika Mashariki,”
Lulu anasema kuwa filamu yake ya Ni Noma ameigiza katika viwango vya
kimataifa na imechukua muda mrefu katika kuandaliwa na anaamini ndio
kazi ambayo itampeleka katika tuzo kubwa za Oscar hata kuibuka kinara
kwani ndio malengo yake.
Filamu ya Ni Noma imetengenezwa na kampuni ya Proin Promotions na
inauzwa kwa njia ya mtandao kupitia Proin Box na inapatikana nchi zote
Duniani ni kazi nzuri sana kwani ndio sinema ya kwanza kushirikisha
wasanii kutoka nchi mbalimbali pia.
No comments:
Post a Comment