Friday, 17 June 2016

BAADA YA AJIRA KUWA TABU HAPA NCHINI,CHINA YAJITOA MHANGA KUAJIRI

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, 

Moja ya stori ambayo imeandikwa June 17 2016 kwenye gazeti la Mwananchi ni hii yenye kichwa cha habari ‘wahitimu wa vyuo vikuu ‘kuula’ China’

Gazeti hilo limeripoti kuwa zaidi ya wahitimu  5000 kutoka vyuo vikuu wanatarajiwa kuajiriwa katika kampuni za Kichina zilizopo nchini China. Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) (Taaluma), Profesa Frolence Luoga alisema chuo hicho na Taasisi ya China ya Confucius, watafanya maonyesho yatakayoenda sambamba na mchujo wa vijana wanaofaa kwa ajiri ya ajira hizo.
Kupitia Gazeti hilo Profesa Luoga alisema katika maonyesho hayo yatakayofanyika kuanzia Juni 18 hadi 19 yatashirikisha zaidi ya Kampuni 100 za China zinazofanya shughuli zake nchini. 
Luoga alifafanua kuwa katika maonyesho hayo wahitimu wanatarajia kujadiliana masuala mbalimbali kuhusu vianda na uchumi, ikiwa ni njia ya kutambua ajira zilizopo.
Aidha gazeti hilo limezungumza na Mtaalamu wa lugha ya Kiswahili wa UDSM, Prof. Aldin Mtembei ambapo amesema wahitimu watakaoshiriki ni kutoka vyuo vyote vya elimu ya juu.
Prof. Mtembei alisema siku ya maonyesho hayo wahitimu hao wanatakiwa kwenda na nakala za wasifu wao (CV), picha na vyeti vinavyoonyesha matokeo yao ya mitihani ili wakiingia kwenye majadiliano na waajiri iwe rahisi kuhakiki sifa zao.

No comments:

Post a Comment