Friday, 24 June 2016

TAZAMA MAJINA YA WANAFUNZI WATAKAO JIUNGA KIDATO CHA TANO 2016/2017


SERIKALI kupitia TAMISEMI imetangaza majina ya wanafunzi watakao jiunga kidato cha tano mwaka 2016
FUNGUA LINK HAPO CHINI

http://tamisemi.go.tz/form_five_selection/

SIASA SASA YAANGWA RASMI,HII NDIYO TAARIFA ILIYOSOMWA NA WATU WENGI ZAIDI LEO BAADA TU YA RAIS KUTANGAZA

June 23 2016 Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekabidhi taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika tarehe 25 Oktoba, 2015 kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa taarifa hiyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kwa sasa uchaguzi umekwisha na ametaka watanzania wote wajielekeze kufanya kazi. 
>>>’Kila nchi hata nchi zenye demokrasia, zilizobobea kwa demokrasia unapokwisha uchaguzi unakuwa ni wakati wa kazi, haiwezekani kila siku ni siasa watu watalima saa ngapi’?

Thursday, 23 June 2016

TAJIRI WA TP MAZEMBE AHUKUMIWA JERA...NINI HATIMA YA ULIMWENGU?????



Mmiliki wa klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Moise Katumbi amehukumiwa kwenda jela, Katumbi ambaye ni boss wa TP Mazembe ambayo ilikuwa inachezewa na nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu.
Katumbi amehukumiwa miaka mitatu sambamba na kutozwa faini ya dola milioni 6 kwa kosa la kujimilikisha eneo, Katumbi pia alikuwa anatajwa kugombea nafasi ya Urais wa Kongo mwishoni mwa mwaka 2016 kupitia chama cha upinzania kushinda na Rais anayemaliza muda wake Joseph Kabila.
rts7qug-e1462504316478
Hata hivyo wakati wa kutolewa hukumu hiyo Moise Katumbi hakuwepo Kongo, siku moja kabla ya hukumu alikuwa kasafiri kwenda Afrika Kusini kupata matibabu, makosa mengina anayotuhumiwa nayo Katumbi ni pamoja na kutajwa kuajiri wa geni kutoka nje ya Kongo kwa ajili ya kuandaa njama za kumuondoa Rais Kabila.
Moise Katumbi ndio Rais wa klabu ya TP Mazembe aliyoingoza kucheza hadi hatua ya fainali ya klabu Bingwa ya dunia dhidi ya Inter Milan December 18 2010, rekodi ambayo hakuna klabu ya Afrika imewahi kuifikia, TP Mazembe ndio ya kwanza, TP Mazembe wanakuja Tanzania June 28 kucheza mchezo wao wa pili wa nane bora dhidi ya Yanga.

Tuesday, 21 June 2016

MIMBA MPYA YA ZARI MASHAKANI!!1

Hii ni habari ya motomoto kabisa! Mama la mama, Zarinah Hassan ‘Zari The  Boss Lady’ amedaiwa kunasa ujauzito wa mpenzi wake, Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Risasi Mchanganyiko lina ubuyu ulionyooka.

Taarifa hizo za ndani ya familia zimevuja ikiwa ni takriban miezi nane tangu mrembo huyo ampe jeuri Diamond ya kutembea kifua mbele kwa kumzalia Tiffah ambapo inaelezwa kuwa, amefanya hivyo makusudi kuwakata ‘vilimilimi wabaya’ wake.Zarimond


TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo makini kutoka ndani ya familia ya Wasafi Classic Baby (WCB), juzikati kilinyetisha kuwa, gumzo la mjini kwa sasa ni wadau wa burudani kujadili ujauzito wa Zari, ambao unaonekana kuwatisha karibia wapambe wote wa timu pinzani.
“Naomba nikudokeze juu ya Zari kuwa mjamzito tena, habari hii ni ya uhakika na kila mtu WCB anajua, Zari amenyaka mimba na cha ajabu amekataa katakata kuichomoa kama Diamond alivyokuwa akimshawishi.

NDIYO CHANZO CHA UGOMVI
“Huwezi kuamini ugomvi wote ambao umekuwa ukidaiwa kuendelea kati ya Diamond na Zari umesababishwa na ujauzito huo ambapo Diamond amekuwa akitumia nguvu nyingi kumuomba Zari achomoe mimba hiyo lakini hakuna hata siku moja ambayo ameonesha dalili za kumuelewa.

MIMBA INA MIEZI MINNE
Chanzo hicho kilizidi kuweka bayana kuwa, kinachomsikitisha Diamond ni kwamba, mimba hiyo inazidi kukua jambo ambalo anaona si sahihi kwa sasa kwani ana mtoto (Tiffah) ambaye bado hajatimiza hata mwaka mmoja.
“Jamaa anaona soo, anaona kama jamii haitamuelewa hivi, jitihada zake za kumshawishi zinagonga ukuta na mbaya zaidi mimba kwa sasa ina kitu kama miezi minne,” kilisema chanzo hicho makini.

SAFARI ZA SAUZ ZATAJWA
Chanzo hicho kilizidi kutiririka kuwa, safari ambazo Diamond alikuwa akizifanya mara kwa mara kwenda Afrika Kusini  (Sauz), nyingi zilikuwa ni za kutatua mgogoro huo ambao umeikumba familia ya WCB, kiasi kwamba hadi wazazi wote wameshirikishwa lakini mwisho wa siku hakuna muafaka.
“Si unakumbuka kuna kipindi Diamond alikuwa anakwenda Sauz mara kwa mara, ishu hiyo ndiyo ilikuwa inampeleka lakini hazikuzaa matunda, mamaa kagoma,” kilisema chanzo hicho.

FAMILIA YAKE YAMSHANGAA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, familia yake imemshangaa Diamond kwa nini hakuwa makini wakati alijua kabisa Tiffah bado angali mdogo.
“Wamemshangaa sana kwa kushindwa kuwa makini wakati kwa sasa kuna mbinu nyingi sana za kuepuka ujauzito, sasa matokeo yake amesababisha hadi kuwe na mvutano unaokosa muafaka,” kilisema chanzo hicho.

NDUGU WA DIAMOND ATHIBITISHA
Mwanahabari wetu alipokuwa akiichimba habari hii, alizungumza na mmoja wa ndugu wa Diamond ambaye alikiri kuwa Zari ni mjamzito lakini akaombwa asitajwe jina maana suala hilo limegubikwa na usiri mzito.
“Ndiyo hivyo kama ulivyosikia. Zari hataki kutoa, nahisi kwa sababu ya kuwakomesha zile timu pinzani lakini anashindwa kujua upande wa pili familia inashindwa kukubaliana naye maana ni jambo la aibu kupata mimba kabla mtoto wa awali hajafikisha hata mwaka,” alisema ndugu huyo.

MSIKIE DIAMOND
Baada ya kupenyezewa ubuyu  huo wa motomoto, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Diamond mwenyewe ili aweze kuweka bayana habari hiyo ya heri, ambapo hakutaka kukataa wala kukubali licha ya kukiri kuzisikia habari hizo.
“Dah! Habari hizi sijui muda mwingine huwa mnazinyaka vipi, sijui hapa niseme nini zaidi ila unachotakiwa kufahamu mimi bado nahitaji kupata watoto zaidi ya mmoja na ifahamike kuwa ninapenda watoto sana, maana uwezo wa kuwahudumia ninao hata hivyo kushika mimba kwa Zari ni mapema sana,” alisema Diamond.

MAMA YAKE NAYE
Mama mzazi wa msanii huyo, Sanura alitafutwa ili kusikia maoni yake, lakini badala yake, aliishia kucheka na kumuomba mwandishi wa habari hizi kuachana na mambo hayo.

Chanzo:Global Publishers

Highlights na goli la mechi ya MO Bejaia vs Yanga June 20, Full Time 1-0

USIKU wa June 20 2016 Dar es Salaam Young Africans walikuwa Algeria kucheza mchezo wao wa kwanza wa Kundi A wa hatua ya nane bora dhidi ya wenyeji wao MO Bejaia, katika mchezo huo Yanga walifungwa na MO Bejaia kwa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa naArmando Sadiku dakika ya 20.

Friday, 17 June 2016

BAADA YA AJIRA KUWA TABU HAPA NCHINI,CHINA YAJITOA MHANGA KUAJIRI

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, 

Moja ya stori ambayo imeandikwa June 17 2016 kwenye gazeti la Mwananchi ni hii yenye kichwa cha habari ‘wahitimu wa vyuo vikuu ‘kuula’ China’

Gazeti hilo limeripoti kuwa zaidi ya wahitimu  5000 kutoka vyuo vikuu wanatarajiwa kuajiriwa katika kampuni za Kichina zilizopo nchini China. Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) (Taaluma), Profesa Frolence Luoga alisema chuo hicho na Taasisi ya China ya Confucius, watafanya maonyesho yatakayoenda sambamba na mchujo wa vijana wanaofaa kwa ajiri ya ajira hizo.
Kupitia Gazeti hilo Profesa Luoga alisema katika maonyesho hayo yatakayofanyika kuanzia Juni 18 hadi 19 yatashirikisha zaidi ya Kampuni 100 za China zinazofanya shughuli zake nchini. 
Luoga alifafanua kuwa katika maonyesho hayo wahitimu wanatarajia kujadiliana masuala mbalimbali kuhusu vianda na uchumi, ikiwa ni njia ya kutambua ajira zilizopo.
Aidha gazeti hilo limezungumza na Mtaalamu wa lugha ya Kiswahili wa UDSM, Prof. Aldin Mtembei ambapo amesema wahitimu watakaoshiriki ni kutoka vyuo vyote vya elimu ya juu.
Prof. Mtembei alisema siku ya maonyesho hayo wahitimu hao wanatakiwa kwenda na nakala za wasifu wao (CV), picha na vyeti vinavyoonyesha matokeo yao ya mitihani ili wakiingia kwenye majadiliano na waajiri iwe rahisi kuhakiki sifa zao.

SIMU FEKI ILIVYO SABABISHA KIFO CHA MAMA YANGU,,,,SEHEMU YA KWANZA

Baada ya kushituka usiku wa manane kutoka na kelele zilizokuwa zimeenea,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,karibu numba yetu,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,nilijikaza na kuamuka huku nikielekea chumba cha ama yangu,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,wakati nafungua mlango ndipo,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,nilipomuona mama yangu akiwa anavuja DAMU nyingi,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,kwa woga ule ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,nilidondoka chini na kuanza kutambaa kuelekea iliko kuwa SIMU YANGU ili nimpigie MJOMBA aliyekuwa jirani na nyumba yetu,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,baada ya kuishika SIMU YANGU,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,ILI KUWA HAINA MTANDAO,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,BILA SHAKA ZOEZI LA KUZIMA SIMU LILIKUWA limenikumba ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,na GIZA LOTE HILI,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,Jamani,,,,,,,,,,,,,,,,kweli mama yangu ANAKUFA MACHONI MWANGU,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,ITAENDELEA

MAJINA MAPYA YA KIKOSI CHA YANGA,KUCHEZAKOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

Shirikisho la Soka Afrika (CAF), limepitisha majina ya wachezaji wanne wapya wa Yanga, kipa Benno Kakolanya, Hassan Ramadhan ‘Kessy’, Vincent Andrew Chikupe na Juma Hassan Mahadhi kucheza Kombe la Shirikisho.
Toa maoni yako

ZAWADI YA SIMU ILIVYOFANYA MPENZI WANGU KUNISALITI,,,,NAOMBA USHAURI

Mpenzi wangu aliniomba nimnunulie simu kali ili tuwasiliane vizuri,
nikamnunulia simu ya laki 6. Juzi nikiwa naye nikaangalia simu yake bila yeye kujua nikakuta kuna jamaa ana mahusiano naye na picha hutumiana na kukutana kinyemela.
Nishaurini nikachukue simu yangu au nivumilie?

MSHAURI HUYU DADA,,,,,,,,,,

MSHAURI HUYU DADA
Niliumizwa sana na mapenzi katika maisha yangu, lakini akaja kutokea mkaka mmoja nikampenda, naye akanipenda, akanifanya nisahau maumivu yote niliyopitia, tatizo huyu mpenzi wangu anavuta sana bangi mpaka naogopa, ila kiukweli ndiye mwanaume pekee aliyenifanya nifurahie mahusiano. Nifanyeje maana nimemshauri kuacha bangi hataki.

MAAMUZI YA MAALIM SEIF AKIWA MAREKANI

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad akiwa nchini Marekani, ataka iundwe serikali ya mpito visiwani Zanzibar itakayokaa kwa muda usiozidi miezi 6 ili uandaliwe uchaguzi mpya visiwani humo, huku akiweka sharti kuwa uchaguzi huo wa marudio usimamiwe na Umoja wa Mataifa badala ya ZEC inayoongozwa na Salim Jecha, pia serikali ya mpito iundwe na watu wasiofungamana na upande wowote wa kisiasa.

ABDU KIBA,,,,,,HUU NDIYO UAMUZI WANGU MPYA kujiunga WBC

Staa wa Bongo Fleva, Abdul Kiba  ametolea ufafanuzi kuhusu taarifa iliyosambaa mitandaoni kujiunga na WCB WASAFI ambayo inamilikiwa na Diamond Platnumz.

Abdul Kiba
Akiaongea na cloudsfm.com Abdul Kiba ambae ni mdogowake na msanii Abdul Kiba alieleza.
‘’Ni kweli nilizungumza hiyo lakini wengi wao waliitafsiri vibaya kauli yangu kwasababu ukizungumzia mtonyo nilimaanisha kwamba nina uwezo wa kufanya nao kazi aidha ikitokea labda ‘featuring’ au kuna shoo naweza nikashirikiana nao kwa sababu ni mkataba utatakiwa upite hapo then pesa imwagike nifanye nao kazi ila siku maanisha kwamba nina uwezo wa kuhama ‘lebo’ kutoka hapa nilipo kwenda kwao, nadhani wengi wao waliipokea kauli yangu vibaya’

NINI KISA CHA MASHAMBULIZI DHIDI YA WOLPER,JE NI HARMONIZE

Chupuchupu! Mwanadada anayeng’ara kunako tasnia ya filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper, juzikati almanusra apigwe risasi kwenye kituo kimoja cha mafuta kilichopo Tegeta (jina linahifadhiwa) jijini Dar es Salaam, baada ya kuibuka kwa timbwili zito eneo hilo, Risasi Mchanganyiko linakupa mkasa mzima.

Tukio hilo la aina yake, lilijiri mishale ya saa tano usiku wa Juni 12, mwaka huu ambapo kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika, Wolper alinusurika kupigwa risasi na mlinzi wa kituo hicho cha mafuta baada ya kutokea hali ya sintofahamu kati yake na mfanyakazi mmoja kwenye kituo hicho.
“Ishu yenyewe ni kwamba, kuna muda Wolper alifika pale sheli (Sheli ni neno lililozoeleka likimaanisha kituo cha mafuta, lakini ukweli ni kuwa jina hilo ni la kampuni ya mafuta yenye makao makuu yake Nchini Marekani) akiwa ndani ya gari aina ya Toyota Mark X, lile linalodaiwa kuwa ni la mpenzi wake wa sasa, Harmonize (Rajab Abdulkan).
“Akaongeza mafuta na kuondoka zake, dakika kadhaa baadaye, tulishangaa kumuona Wolper akirudi tena na kwenda mpaka kwa yule dada aliyemuuzia mafuta lakini safari hii alionekana kuja kwa shari.
“Akashuka kwenye gari na kuanza kumuwakia yule dada kwa madai kwamba amemuibia mafuta na kusababisha gari lake limzimikie njiani wakati alitoa shilingi elfu ishirini,” kilisema chanzo chetu.
Kwa mujibu wa chanzo, timbwili la aina yake lilizuka eneo hilo baada ya msichana huyo kuanza kumjibu mbovu msanii huyo ambaye hakukubali, Wolper akakinukisha kwa kumvaa na kuanza kumshushia kichapo, tukio lililokusanya umati wa watu.
Ilibidi mlinzi wa kituo hicho cha mafuta, aingilie ugomvi huo. Hata hivyo, mlinzi huyo alionekana kumtetea zaidi mfanyakazi mwenzake na kumkandamiza Wolper, jambo lililozidi kumpa hasira msanii huyo.
“Alipoona wanasaidiana, Wolper aliwachenjia wote wawili, jambo lililosababisha mlinzi huyo aondoke eneo hilo lakini aliporejea, alikuwa na bunduki yake ya lindo mkononi, akaikoki na kutaka kumpiga risasi Wolper,” kilisema chanzo chetu na kuongeza kuwa kuona hivyo, Wolper alikimbilia ndani ya gari lake na kutoka nduki, akiacha watu wengi wakiwa wamekusanyika kituoni hapo.
Baada ya kusikia maelezo hayo kutoka kwa chanzo chetu, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Wolper ambaye baada ya kusomewa mashtaka hayo, alikiri kutokea kwa tukio hilo.
“Dah, ni kweli nilikutana na matatizo hayo usiku, ambapo nilikuwa naenda Tegeta baada ya kufika njiapanda flani pale, gari lilipungua mafuta nikaingia kituoni na kuongeza ya elfu 20, wakati naongeza nilihisi kabisa yule dada ananiibia lakini sikumjali, nikalipa na kuondoka.
Nilipofika mbele kidogo tu gari lilizima,” alisema Wolper na kuongeza: “Ilibidi nifanye utaratibu wa kupata mafuta mengine kisha nikageuza na kurudi mpaka pale sheli kwa lengo la kudai haki yangu ndiyo kukatokea timbwili hilo kwani mlinzi wa pale alikuwa anamsaidia yule dada aliyeniibia.”
“Wakati nikiwa najihami maana yule mlinzi alikuwa akinikaba, nilimpiga kibao, akakimbilia bunduki yake na kuanza kuikoki akitaka kunipiga risasi.
“Baada ya kuona amefikia hatua hiyo niliingia haraka kwenye gari langu na kuondoka zangu kwani nilihisi walikuwa na njama moja ya kuniibia mafuta na walipoona nimerudi kulalamika ndiyo wakaamua kunifanyia vurugu, kweli sikufurahishwa na tabia yao kwanza ni wezi wakubwa wa mafuta hao,” alisema Wolper.

LULU,NIPO KIMATAFA ZAIDI

ELIZABETH Michael ‘Lulu’ mwigizaji wa kike mwenye nyota kali anasema kuwa hawezi kwa sasa kuonekana kwa kila filamu bila sababu kwani amejipanga kutafuta tuzo kubwa za kimataifa hivyo lazima ashiriki sinema bora ili kufikia malengo yake.


“Kuwa bora si kucheza sinema nyingi bali kuwa na sinema za maana, nimejipanga na nakuja na filamu yangu ya Ni Noma ni filamu kubwa sana kutengezwa Afrika Mashariki,”
Lulu anasema kuwa filamu yake ya Ni Noma ameigiza katika viwango vya kimataifa na imechukua muda mrefu katika kuandaliwa na anaamini ndio kazi ambayo itampeleka katika tuzo kubwa za Oscar hata kuibuka kinara kwani ndio malengo yake.
Filamu ya Ni Noma imetengenezwa na kampuni ya Proin Promotions na inauzwa kwa njia ya mtandao kupitia Proin Box na inapatikana nchi zote Duniani ni kazi nzuri sana kwani ndio sinema ya kwanza kushirikisha wasanii kutoka nchi mbalimbali pia.

Friday, 3 June 2016

7 WAYS TO KNOW YOUR PARTNER JUST SLEPT WITH SOMEONE ELSE


The issue of infidelity in relationships can never be overlooked as it is a subject that affects many. The same way women cheat in relationships, men also cheat
What most people fail to understand is that there would always be lapses when a party starts to cheat on the other person. Although, many would agree that catching a cheating partner is psychological; this explains why people say their instincts led them to the discovery. In this piece, we would be looking at the signs men watch out for when they want to know if their woman has been cheating or not. The signs that would be raised would be considered elementary for those girls who make cheating their life ambition and would never be caught doing it. Find below some of the give-away signs that men watch out for when women cheat on them:
            CLICK BELOW TO WATCH

RAYMOND NATAFUTAKIKI LISTER A SONG

A NEW SONG


RICH MAVOKO IBAKI STORY

A BRAND NEW SONG BY Rich MAVOKO after signing a new contract with WBC  LABEL