Serikali imekifungia kituo cha tiba asilia cha Foreplan kinachomilikiwa na Juma Mwaka kwa kukiuka masharti ya kibali alichopewa kujitangaza kuwa anatoa tiba za kisasa badala ya matibabu ya asilia.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam,
Mwenyekiti Wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Dk Edmund Kayombo
amesema kuwa kituo hiko kimefutiwa usajili na hakiruhusu kutoa huduma za
tiba asilia na tiba mbadala kwa jamii kwa kutokidhi masharti ya usajili
na kufanya kazi kinyume cha usajili wake.
“Kuanzia hivi sasa tumekifutia usajili kituo cha tiba asili na tiba
mbadala cha Foreplan kwa kukiuka masharti ya usajili na hivyo
hakiruhusiwi kutoa huduma kwa jamii na watanzania kwa
ujumla,”amesisitiza Dk Kayombo.
Ameongeza kuwa vituo vingine vilivyofungiwa kutoa huduma ni pamoja na
Tabibu Abdallah Mandai wa Mandai Herval Clinic na Kituo cha Fadhaget
Sanitarium Clinic kinachomilikiwa na Tabibu Fadhil Kabujanja
No comments:
Post a Comment