Wednesday, 13 July 2016

MSEVENI AFANYA KITUKO CHA MWAKA,TAZAMA

Museveni asimamisha msafara kisha aketi barabarani kuzungumza na simu.



Rais wa Uganda bwana Yoweri Kaguta Museveni alizua kihoja katika kijiji kimoja karibu na mpaka wa Uganda na Tanzania aliposimamisha msafara wake wa magari iliapokee simu faraghani.
Amini usiamini Rais Yoweri Museveni, alishuka kutoka kwenye gari lake rasmi akachukua kiti chake na kukiweka kando kando ya barabara mpya ya Isingiro ikipitia kijiji hicho cha Kyeirumba hadi Tanzania na kupokea simu faraghani.

Mzee Museveni kama vile baba wa taifa alitumia muda wake kufanya shughuli hiyo huku akiwapungia mkoo wapita njia.

DK MWAKA AFUNGIWA RASMI-HIZI NDIZO SABABU KUU



Serikali imekifungia kituo cha tiba asilia cha Foreplan kinachomilikiwa na Juma Mwaka kwa kukiuka masharti ya kibali alichopewa kujitangaza kuwa anatoa tiba za kisasa badala ya matibabu ya asilia.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Mwenyekiti Wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Dk Edmund Kayombo amesema kuwa kituo hiko kimefutiwa usajili na hakiruhusu kutoa huduma za tiba asilia na tiba mbadala kwa jamii kwa kutokidhi masharti ya usajili na kufanya kazi kinyume cha usajili wake.
“Kuanzia hivi sasa tumekifutia usajili kituo cha tiba asili na tiba mbadala cha Foreplan kwa kukiuka masharti ya usajili na hivyo hakiruhusiwi kutoa huduma kwa jamii  na watanzania kwa ujumla,”amesisitiza Dk Kayombo.
Ameongeza kuwa vituo vingine vilivyofungiwa kutoa huduma ni pamoja na Tabibu Abdallah Mandai wa Mandai Herval Clinic na Kituo cha Fadhaget Sanitarium Clinic kinachomilikiwa na Tabibu Fadhil Kabujanja

MZIMU-WAANUA UNGA WA UGALI MBEYA

Mzimu wa ajabu waanua unga wa ugali

 



Na Ibrahim Yassin, Rungwe
WANANCHI  wa Kijiji  cha  Mwela  Kata  ya  Kandete  wilayani  Rungwe Mkoa wa Mbeya wako hatarini kukumbwa na baa la njaa baada ya kuibuka kile kinachodaiwa ‘mzimu wa ajabu’ ambao umekuwa ukianua unga  unapokuwa umeanikwa juani na kupotea hewani katika mazingira ya kutatanisha.
Hali  hiyo  imejitokeza  siku  chache baada ya ‘mzimu’ huo kuzuka  katika kijiji hicho   ikielezwa kuwa unga na mazao mengine yaliyokuwa yameanikwa juani yalipotea hewani.
Kutokana na tukio hilo,   imewalazimu wananchi wa Kijiji cha Mwela kutisha mkutano wa halmashauri ya kijiji   kujadili na kutafuta suluhu ya hali hiyo.
Akizungumza na mwandishi   kuhusu tukio hilo, mkazi mmoja wa kijiji hicho, Hamfrey Mwakitwange, alisema kuibuka kwa mzimu huo kumezua hofu kwa wakazi wa Mwela na maeneo ya jirani.
Alisema   mwaka huu kuna hatari ya kutokea  ukame na  baa la njaa    baada ya kuibuka   mzimu huo wa ajabu.
“Kwa tukio la kuwapo   mzimu huu wa ajabu tumejawa na hofu kubwa   na kuna dalili ya kukumbwa na baa la njaa mwaka huu.
“Mzimu umekuwa ukichukua chakula hasa unga na mazao yanayoanikwa juani…tunabaki tunajiuliza, na sasa kimeitishwa kikao cha halmashauri ya kijiji ingawa mtazamo umegawanyika… sasa kuna wengine wanataka hata tuhushishe waganga,” alisema Mwakitwange.
Mjumbe wa Nyumba 10 wa CCM, Matrida Mwaisumbwa, alisema   kitendo cha kuibuka   mzimu huo ambao umekuwa ukichukua chakula,  umeleta sintofahamu kijijini hapo.
Alisema   hata wanapokuwa wanapika chakula kama ugali au ndizi, kimekuwa hakina radha   na inadaiwa chakula hicho pia kinakuwa kimetembelewa na mzimu huo wa ajabu.
Alisema uongozi umeandaa mkakati wa kupita nyumba kwa nyumba   kukusanya michango  kuwasaidia wananchi ambao wamekwisha kuathirika na mzimu huo.
Hata hivyo,  Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwale, Ferki  Mwandenga, alisema licha ya kuwapo taarifa za mzimu huo wa ajabu  anashindwa kuieleza kwa kina hali hiyo.
“Siwezi kulisema hili jambo maana linachanganya kidogo, sijui ni tukio la kichawi? Ingawa pamoja na hali hiyo, tambua kuwa Serikali haiamini uchawi,” alisema Mwandega.

JULIO-WACHEZAJI WA KIGENI SIYO DILI

Julio aponda usajili wachezaji wa kigeni

 


Jamhuri Kihwelu ‘Julio’
NA THERESIA GASPER, DAR ES SALAAM
KOCHA Mkuu wa timu ya Mwadui FC, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’, amesema hababaishwi na usajili wa wachezaji wa kimataifa unaofanywa na baadhi ya klabu zitakazoshiriki Ligi Kuu Bara msimu ujao na kudai kuwa ana uwezo wa kupata wachezaji wazawa wenye viwango vya juu zaidi.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Julio alisema anaamini wapo wachezaji wazawa wenye uwezo kwani baadhi yao viwango vinalingana na ambao wanasajiliwa kutoka nje ya nchi.
“Wachezaji wa nje ambao nakubali viwango vyao ni Thabani Kamusoko, Donald Ngoma na Haruna Niyonzima wa Yanga pamoja na Kipre Tchetche wa Azam FC, lakini wengine wana uwezo wa kawaida,” alisema.
Julio aliyeipandisha Mwadui Ligi Kuu na kuiwezesha kubaki msimu uliopita, alisema atafanya usajili wa wachezaji wazawa wenye uwezo ambao anaamini watakiimarisha kikosi na kuongeza ushindani msimu ujao.
Akizungumzia tetesi za kutaka kumsajili kiungo aliyetemwa na Yanga, Salum Telela, Julio alikiri kufanya naye mazungumzo na kudai kilichobaki ni mchezaji huyo kufanya uamuzi.

Sunday, 10 July 2016

WACHEZAJI WA YANGA WALINYOAMUA KUTOA ZAWADI

Timu ya Yanga inayojiandaa na mchezo wake wa tatu wa Kombe la shirikisho Afrika dhidi ya Medeama ya Ghana, Jumapili July 10 ilitembelea kwa mdhamini wao kampuni ya Quality Group kwa ajili ya kutoaa zawadi.
Baadhi ya mastaa wa Yanga waliotoa zawadi kwa mashabiki na kupiga nao picha ni Malimi Busungu, Nadir Haroub Canavaro, Thabani Kamusoko na Donald Ngoma ambapo ni mpira na jezi vilivyosainiwa na wachezaji wote na pikipiki kwa mshindi wa kwan

MAMA YAKE RONALDO,ALIANDIKA HAYA BAADA YA KUONA MWANAE AKILIA

Usiku wa July 10 2016 mchezo wa fainali ya Euro 2016 ulichezwa na kushuhudia timu ya taifa ya Ureno ikifanikiwa kutwaa Kombe la Euro kwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya mwenyeji Ufaransa.
Tukio la kuumiza kwa mashabiki wa Ureno ni pale dakika ya 23 nahodha wao Cristiano Ronaldo alipotolewa nje ya uwanja kwa kubebwa juujuu akiwa analia baada ya kushindwa kuendelea na mechi kutokana na kufanyiwa faulo mbaya.
roiu
Muda mfupi baada ya Ronaldo kutolewa analia, mama mzazi wa staa huyo Dolores Aveiroaliandika ujumbe wake kutumia account yake ya twitter unaoonesha kusikitishwa kwake kwa faulo aliyofanyiwa mwanae Siwezi kumuangalia mwanangu akiwa katika hali hii (analia), kucheza mpira sio kumuumiza mpinzani”

Monday, 4 July 2016

ORGANIZE HONEYMOON- TOURS and SAFARI -

 WE ORGANIZE
HONEYMOON- TOURS and SAFARI -


ZANZIBAR /TANZANIA
BOOK TODAY +255 754 441368 (Whtsapp)
>+255 712 41 31 41
EMAIL- paschal@theinsighttanzaniasafaris.com
#toursintanzania
#zanzibartour
#kilimanjarotours
#lakezonetours